Mfanyabiashara Mohamed Dewji (MO) ameongea na muheshimiwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na amemuhahidi mambo haya:
1.Kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza sabuni ya unga ambacho kitakuwa ni kikubwa kuliko vyote katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.
2.Kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda cha sukari katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.
3.Kuwekeza sh. bilioni 40 kwa ajili ya kukuza uzalishaji katika mashamba yake ya mkonge kwenye mikoa ya Pwani, Tanga na Morogoro.
4.Tayari amewekeza sh. bilioni 70 katika viwanda vya kusaga unga wa ngano na sembe na anatarajia kununua tani laki moja za mahindi katika msimu wa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment