RAIS John
Magufuli amesema binadamu wanatakiwa kuwa na umoja hata kama wana tofauti
mbalimbali zikiwamo za kimadhehebu ya dini, siasa na kanda, huku akiwaomba
viongozi wa dini kuendeleza juhudi zao za kuliombea taifa na kuwaunganisha
wananchi licha ya tofauti zilizomo miongoni mwao.
Rais
Magufuli alitoa kauli hiyo jana baada ya kumalizika kwa Misa Takatifu ya
kuadhimisha Jubilee ya miaka 50 ya Ndoa ya Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu,
DR.Benjamin William Mkapa na mkewe, Anna Mkapa iliyofanyika kwenye Kanisa la
Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment