WALIMU WA SHULE YA MBEYA SECONDARY WAMSHAMBULIA MWANAFUNZI NA KUMPIGA SANA
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida, walimu wa shule ya mbeya secondary wamempiga mwanafunzi ambaye aligoma kupewa adhabu.
Hali hii imejitokeza shuleni hapo ambapo wanafunzi hawakufanya vizuri kwenye masomo yao ndipo mwalimu alipoamua kutoa adhabu kwa darasa zima. Mwanafunzi huyo aligoma kuadhibiwa kutokana na madai ya kuwa matokeo yake hakutendewa haki.
Hivyo kwakuwa aligoma kupewa adhabu, walimu hao walimpeleka ofisini, na hicho ndicho kilichomtokea.
Kupitia mtandao wa instgram , Waziri wa mambo ya ndani mhe: Mwigulu Nchemba amesikitishwa sana na jambo hili na ametoa maagizo kwa watu wanaohusika na maswala ya mitandao wawatafute watu waliofanya tukio hili mara moja.
No comments:
Post a Comment