Tenzi za Rohoni – 77 MSALABANI PA MWOKOZI
1.Msalabani pa mwokozi, Hapo niliomba upozi, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.
2.Chini ya mti msumbufu, Niliomba utakatifu, Alinikomboa kwa damu, Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Alinikomboa kwa damu, Mwana wa Mungu.
3.Aliniokoa dhambini, Ikawa kunikaa ndani, Aliponifia mtini, Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Aliponifia Mtini, Mwana wa Mungu.
4.Damu ya Yesu ya thamani, Huniokoa makosani, Huniendesha wokovuni, Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Huniendesha wokovuni, Mwana wa Mungu.
5.Hicho kijito cha gharama, Leo jivike kwa kuzama, Kwake uuone uzima, Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Kwake uuone uzima, Mwana wa Mungu.
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
1.Mteteeni Yesu, Mlio askari; Inueni beramu, Mukae tayari, Kwenda nae vitani, Sisi
hatuchoki Hata washindwe pia Yeye amiliki.
2.Mteteeni Yesu, Vita ni vikali; Leo siku ya Bwana, Atashinda kweli, Waume twende naye,
Adui ni wengi, Lakini kwake Bwana Tuna nguvu nyingi.
3.Mteteeni Yesu, Wenye ushujaa; Nguvu zenu za mwili Hazitatufaa; Silaha ya injili Vaeni
daima, Kesheni mkiomba, Sirudini nyuma.
4.Mteteeni Yesu, Vita ni vikali, Wengi wamdharau, Hawamkubali, Ila atamiliki Tusitie shaka,
Kuwa naye vitani Twashinda hakika
No comments:
Post a Comment